Home KIMATAIFA SIMBA QUEENS JE KUWEKA HISTORIA LEO??

SIMBA QUEENS JE KUWEKA HISTORIA LEO??

0

Kocha Mkuu Charles Lukula, amesema kikosi kiko tayari kuikabili Bayelsa Queens kutoka Nigeria kwenye mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika utakaopigwa leo saa nne usiku katika Uwanja wa Prince Heritier Moulay.

Lukula amesema kikosi kipo kamili hata wachezaji waliopata maumivu kwenye mechi zetu zilizopita wapo vizuri na wamefanya mazoezi pamoja na wenzao.

Lukula ameongeza kuwa itakuwa mechi ngumu lakini tunahitaji kushinda ili kuwapa furaha Wanasimba na Watanzania kwa ujumla.

“Maandalizi yamekamilika, nashukuru kwa sasa wachezaji wote wamefanya mazoezi hata wale waliokuwa wamepata maumivu kwenye mechi zetu zilizopita kwa hiyo tutakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi,” amesema Lukula.

Kiungo mkabaji Vivian Corazone amesema baada ya kukosa nafasi ya kucheza fainali sasa tumehamishia nguvu katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Bayelsa.

“Sisi wachezaji tujo tayari kwa mchezo wa kesho {leo}, malengo yetu yalikuwa kufika fainali lakini imeshindikana sasa tunahitaji kupata nafasi ya tatu. Tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tupo tayari kupambana,” amesema Corazone.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here