Home KITAIFA SIMBA YAANZA KUZITAFUTA 5-0 ZINGINE KWA AJILI YA SINGIDA BIG STARS

SIMBA YAANZA KUZITAFUTA 5-0 ZINGINE KWA AJILI YA SINGIDA BIG STARS

0

Baada ya kushinda mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kikosi cha Simba kimeingia kambini leo mchana jumatano kujiandaa na mchezo mwingine wa ligi.

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kiliichapa Mtibwa Sugar Oktoba 30, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba inatarajia kucheza mchezo ujao wa ligi kuu Novemba 9 mwaka huu dhidi ya Singida Big Stars kwenye Uwanja wa Liti, Singida.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema kikosi chao kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wao unaofuata dhidi ya Singida Big Stars.

“Kikosi chetu kimeingia kambini leo jumatano kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Singida Big Stars.

“Mchezo utakuwa mgumu lakini muhimu kwetu ni pointi tatu za kuhakikisha kwamba tunakuwa sehemu salama kwenye msimamo wa ligi.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here