Home KITAIFA SIMBA YASEPA NA POINTI MBELE YA NAMUNGO

SIMBA YASEPA NA POINTI MBELE YA NAMUNGO

0

MOSES Phiri nyota wa Simba amefunga bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Ulikuwa ni mchezo wa wazi kwa timu zote mbili kusaka ushindi ambapo kipindi cha kwanza Simba walimaliza mchezo kwa kupata bao la ushindi.

Ilikuwa ni dakika ya 32 Phiri alipachika bao hilo na kuipa pointi tatu Simba akitumia pasi ya Mohamed Hussein Zimbwe Jr.

Namungo walikuwa imara kipindi cha pili ambapo kuingia kwa mshambuliaji wao namba moja Relliats Lusajo kuliongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Lusajo alipiga mashuti mawili yaliyolenga lango ikiwa ni dakika ya 88 na 90 lakini alikwama kufunga mbele ya Aishi Manula.

Simba inafikisha pointi 24 baada ya kucheza mechi 11 za ligi msimu wa 2022/23.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here