Home KITAIFA SINGIDA BIG STARS V SIMBA BALL LIMETEMBEA

SINGIDA BIG STARS V SIMBA BALL LIMETEMBEA

0

HILO ball lililopigwa Uwanja wa Liti ni viwango vyajuu huku Simba wakipigishwa kwata ndani ya dakika 90 kutoka kwa walima alizeti Singida Big Stars.

Kipindi cha kwanza walishuhudia bao la kwanza kutoka kwa Deus Kaseke aliyetumia pasi ya Said Ndemla dakika ya 11 likiwa ni bao la mapema kwa Simba kufungwa.

Iliwabidi Simba wasubiri kipindi cha pili kupata bao kupitia kwa Peter Banda dakika ya 58 na kuwanyanyua mashabiki wa Simba.

Umakini hafifu kwa washambuliaji wa Simba ikiwa ni pamoja na Moses Phiri na Kibu Dennis utawafanya wajilaumu wenyewe.

Kwa upande wa Singida Big Stars walikosa utulivu wa kutumia afasi wanazopata huku nyota Mangalo akiwa mmoja wa mabeki waliotibua mipango ya wapinzani wao Simba.

Dakika 90 ubao wa Uwanja wa Liti unasoma Singida Big Stars 1-1 Simba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here