Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA LEO ULAYA JUMATATU (14.11.2022)

TETESI ZA SOKA LEO ULAYA JUMATATU (14.11.2022)

0

Mtendaji mkuu wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke anasema klabu hiyo itafanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, ambaye amekuwa akihusishwa na timu kadhaa kubwa za Ulaya, kuhusu mustakabali wake baada ya Kombe la Dunia la 2022. (Bild, via Mail)

Barcelona, ​​ambao wanajua itakuwa vigumu kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 32, kutoka Manchester City mwezi Januari, pia wanamtazama kiungo wa kati wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans, 25. (AS Mundo Deportivo).

Barcelona ilishindwa kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini rais wa klabu hiyo ya Nou Camp Joan Laporta anasema hajatilia shaka nafasi ya Xavi kama meneja. (Sport – In Spain)

Mkufunzi wa Aston Villa Unai Emery anataka kusajili wachezaji wawili kutoka Real Madrid – winga wa Ubelgiji Eden Hazard, 31, na mlinzi wa Uhispania Nacho Fernandez, 32. (El Nacional – In Spain .

AC Milan wanalenga kukubaliana na Chelsea kumsajili winga wao wa Morocco Hakim Ziyech mwenye umri wa miaka 29 mwezi Januari. (Gazzetta dello Sport, Via Football Italia)

AC Milan haitazingatia ofa za chini ya euro 100m (£87.5m) kwa fowadi wa Ureno Rafael Leao mwezi Januari huku wakihangaika kupiga hatua katika mazungumzo ya kuafiki kuongeza mkataba na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Calciomercato – Via Italy)

Mkurugenzi wa Roma Tiago Pinto “hawezi kukubali” hoja ya meneja wa Uingereza Gareth Southgate ya kumuacha mshambuliaji Tammy Abraham, 25, nje ya kikosi chake kwa ajili ya Kombe la Dunia la 2022. (DAZN, Via Football Italia)

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, ambaye aliondoka Chelsea na kujiunga na Real Madrid msimu wa joto, anasema Barcelona walijaribu kumsajili lakini kuhamia Nou Camp haikuwa uwezekano kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (AS – In Spain )

Kiungo wa kati wa Italia Marco Verratti, 30, anakaribia kusaini mkataba wa nyongeza hadi 2026 na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain.(Mundo Deportivo – As Spain ).

Mkataba wa mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko na Inter Milan unamalizika msimu ujao wa joto na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 anasema anataka kusalia na timu hiyo ya Serie A. (Calciomercato – Via Italy)

 

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here