Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA (27.11.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA (27.11.2022)

0

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, amepewa ofa ya mkataba wa mnbono wa miaka mitatu wenye thamani ya £186m na klabu ya Saudi Arabia Al Nassr. (CBS)

Bayern Munich wameingia katika mbio za kumsajili kiungo wa kati wa West Ham na Emngland Declan Rice, 23. (El Nacional, via Fichajes – in Spanish)

Tottenham bado hawajaanza mazungumzo na nahodha na mshambuliaji wa England Harry Kane kuhusu mkataba mpya, huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika msimu wa joto wa 2024.

Spurs italazimika kumpa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 mkataba wa “ajabu” ili kumbakisha. (Football Insider)

Meneja Erik ten Hag ameiomba Manchester United kufanya usajili katika dirisha la Januari kumpata nafasi ya Ronaldo baada ya kuondoka kwake. Katika orodha fupi ya usajili ya klabu hiyo yumo winga wa PSV na Uholanzi Cody Gakpo, 23, na mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23. (ESPN)

Liverpool pia wako tayari kutumia pesa nyingi katika usajili mnamo Januari, licha ya kutokuwa na uhakika kuhusu umiliki wa kilabu. (Football Insider)

Manchester United wamerudi nyuma katika kinyang’anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund. (Sky Sports Ujerumani)

Kamishna wa Ligi Kuu ya Soka Don Garber amethibitisha kuwa vilabu kadhaa katika ligi kuu ya Marekani vina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, wakati mkataba wake wa Paris St-Germain utakapokamilika mwishoni mwa msimu. (90Min)

Beki wa kushoto wa Barcelona Mhispania mwenye umri wa miaka 19 Alejandro Balde ameitaja Manchester United kuwa klabu ambayo angependa kuichezea ukiacha timu yake ya La Liga. (Mundo Deportivo)

West Ham na Everton wamejiunga katika harakati za kuwania saini ya winga wa Colombia Jhon Duran mwenye umri wa miaka 18 kutoka Chicago Fire, lakini Liverpool na Manchester United pia wanamtaka. (Sun)

Tottenham wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Juventus na Marekani Weston McKennie, 24, baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia. (CBS, via Express)

Leeds United, Everton, West Ham na Leicester City ni miongoni mwa klabu zinazomtaka mshambuliaji wa Senegal Boulaye Dia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Salernitana kutoka Villarreal. (CBS)

Leicester, Brighton na Nottingham Forest wanataka kumsajili kiungo wa Huddersfield Mfaransa Etienne Camara, 19. (Sun)

Meneja wa Barcelona Xavi anasema binafsi amezungumza na kinda wa Palmeiras Endrick mwenye umri wa miaka 16 katika nia ya kumshawishi mshambuliaji huyo wa Brazil kujiunga na klabu hiyo ya La Liga. (ESPN)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here