Mkataba wa Januari huenda unaandaliwa na Liverpool kumsajili kiungo wa kati wa England Jude Bellingham kutoka Borussia Dortmund, 19. (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Liverpool Emile Heskey anasema The Reds “wanamwinda” Bellingham. (Mirror)
Liverpool na Juventus wanafuatilia mazungumzo ya kandarasi yanayoendelea kati ya kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 23, na Chelsea. (Guradian)
Chelsea inamwona Mount kama nahodha wa siku zijazo wa klabu lakini mkataba wake wa sasa unaifanya Blues Academy kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa mshahara wa chini zaidi kwenye kikosi hicho. (Mail)
Kocha wa zamani wa Tottenham, Southampton na Paris St-Germain Mauricio Pochettino anasema “atakuwa wazi kwa kila kitu” alipoulizwa kama angependa kuwa meneja wa Uingereza. (Athletic Sunscription Required)
Fulham, Bayer Leverkusen na Villarreal wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Ureno Cedric Soares, 31, kutoka Arsenal mwezi Januari. (ESPN)
Aston Villa ilikataa nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha kabla ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kujiunga na Fulham. (Football Insider)
Mshambulizi wa zamani wa Barcelona na Liverpool Luis Suarez, 35, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Gremio ya Brazil mara tu mkataba wake na Nacional ya nchini kwao Uruguay utakapokamilika. (Fabrizio Romano)
Timu ya taifa ya Poland ilisindikizwa na ndege za kivita kuelekea Qatar kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia. (Sky Sports)
Argentina na Uruguay kila moja imechukua kilo 900 za nyama hadi Qatar ili wachezaji na wafanyikazi waweze kula chakula cha nyumbani wakati wa Kombe la Dunia. (ESPN)
Raia wa Qatar wanataka Fifa kubatilisha uamuzi wa kuruhusu bia kuuzwa katika viwanja vyote vitakavyoandaa mechi za Kombe la Dunia. (Times – subscription Required)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE