Home KIMATAIFA TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE (08.11.2022)

TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE (08.11.2022)

0

Wamiliki wa Liverpool Fenway Sports Group watamsajili kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya £87m kama zawadi ya kuagana kabla ya kuiuza klabu hiyo. (Marca, via FourFourTwo)

Manchester United ni miongoni mwa klabu zinazowania kuinasa saini ya Bellingham, huku Chelsea ikiwa si miongoni mwa timu anazotaka kujiunga nazo. (TeamTalk)

FSG watapata faida kubwa katika uwekezaji wao, lakini thamani ya Liverpool iko chini ya bei ambayo Roman Abramovich aliiuza Chelsea mapema mwaka huu. (Star)

Bilionea wa Uingereza Sir Jim Ratcliffe ni miongoni mwa watu wanaoweza kuinunua Liverpool. (Liverpool Echo)

Mkufunzi wa Luton Town Nathan Jones anatazamiwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Southampton baada ya klabu hiyo ya Ligi kuu England kumfuta kazi Ralph Hasenhuttl siku ya Jumatatu. (Barua)

Southampton wanavutiwa na bosi wa Brentford Thomas Frank na pia walimjadili meneja wa River Plate Marcelo Gallardo. (Guardian)

Zaidi ya nusu ya wawakilishi wa klabu za ligi kuu England walifuatilia mchezo wa Ajax dhidi ya PSV Eindhoven Jumapili, huku winga wa PSV wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, akiwa miongoni mwa wachezaji waliocheza. (90Min)

Matumaini ya Chelsea kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, 23, yameongezeka kwa sababu ya matatizo yanayoendelea katika mazungumzo ya kuongeza mkataba wa mchezaji huyo. (Sky Italy, via Mirror)

Arsenal na Tottenham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Lille raia wa Canada Jonathan David, 22. (GiveMeSport, via TeamTalk)

Vinara wa Ligi ya England Arsenal wako tayari kutumia fedha katika dirisha la uhamisho la Januari ili kuendeleza changamoto yao ya kuusaka ubingwa. (90Min)

Manchester United wanataka kumsajili mshambuliaji wa Bayern Munich na Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting mwezi Januari lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anataka kusalia katika klabu hiyo ya Bundesliga. (Florian Plettenberg)

Mchambuzi na mtaalamu wa kikosi cha kwanza cha Brentford Jack Wilson anaondoka The Bees na kujiunga na mabingwa watetezi wa EPL Manchester City. (Athletic)

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here