Southampton imeamua kumfukuza kazi meneja Ralph Hasenhuttl baada ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Newcastle siku ya Jumapili na kuiacha klabu hiyo katika hatari ya kushuka daraja. (Athletic)
Newcastle United na Aston Villa zinataka kumrejesha ligi kuu ya England mshambuliaji wa Real Madrid na Ubelgiji Eden Hazard, 31. (El Nacional)
Tottenham wanafikiria kumnunua winga wa Everton Muingereza Anthony Gordon, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sun)
Arsenal bado inataka kumsajili winga wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Mykhaylo Mudryk, 21. (CaughtOffside)
Mshambulizi wa RB Leipzig Mfaransa Christopher Nkunku, 24, yuko tayari kuisubiri kwanza Real Madrid kabla ya kuamua kama atahamia Chelsea. (El Nacional)
Arsenal iko katika harakati za kuwaonhezea mikataba mipya mlinzi wa Ufaransa William Saliba, 21, winga wa Uingereza Bukayo Saka, 21, na mshambuliaji wa Brazil Gabriel Martinelli. (Fabrizio Romano)
Mkurugenzi wa PSV Eindhoven Marcel Brands amesema Leeds ilitoa ofa ya £30m pamoja na £11m kama bonasi kwa winga wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, katika dirisha la msimu uliopita wa joto. (ESPN – kwa Kiholanzi)
Mshambulizi wa Lille na Canada Jonathan David, 22, anafuatiliwa na klabu kadhaa za Ligi kuu England zikiwemo Everton, Tottenham na Arsenal. (NipeSport)
Mshambulizi wa Brentford Ivan Toney, 26, yuko tayari kwenda Kombe la Dunia akiwa na England licha ya kuchunguzi na FA kuhusu kushiriki kamari. (Sun)
Winga wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 29, anakataa kubashiri juu ya mustakabali wake licha ya kandarasi yake kumalizika msimu wa joto. (Sky Sports)
West Ham wanapanga kumnunua mshambuliaji wa Blackburn Rovers na Chile Ben Brereton Diaz, 23 katika dirisha lijalo la mwezi Januari (Football Insider)
Leeds inaongoza katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Birmingham, 18, Muingereza George Hall. (Sun)
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE