Home KITAIFA YANGA NGOMA NGUMU MBELE YA WAARABU

YANGA NGOMA NGUMU MBELE YA WAARABU

0

MCHEZO wa mtoano Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa Uwanja wa Mkapa, Yanga imekubali ubao kusoma 0-0 Club Africain na kufanya ngoma kuwa ngumu ikiwa nyumbani.

Ulikuwa ni mchezo wazi kwa timu zote mbili ambazo zilikuwa kwenye msako wa ushindi kupiga hatua moja kuelekea kwenye hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho.

Kete ya kwanza ya Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi imekamilisha dakika 90 za awali bilakuambulia bao ikiwa nyumbani na mashabiki wake.

Kazi iliyopo mbele ni kusaka ushindi ugenini nchini Tunisia mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa utaamua hatma ya nani atakayesonga mbele.

Nyota wa Yanga, Khalid Aucho, Bernard Morrison na Fiston Mayele ni miongoni mwa wale ambao walianza kikosi cha kwanza.

Kwa upande wa mapigo ya mipira iliyokufa jukumu hilo lilikuwa kwenye miguu ya Aziz KI ambaye naye alikwama kujaza mpira nyavuni.

Mchezo huo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Jumatano ya Novema 9, 2022

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here