Home KITAIFA YANGA: WACHEZAJI WAMEKUBALIANA KUFANYA KWELI KIMATAIFA

YANGA: WACHEZAJI WAMEKUBALIANA KUFANYA KWELI KIMATAIFA

0

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa wachezaji wote wamekubaliana kufanya vizuri kwenye mechi za mtoano ili kufika mbali kimataifa.

Yanga leo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa mtoano dhidi ya Club Africains mchezo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa wachezaji wote wana morali kubwa kuelekea mechi zao za kimataifa na malengo ni kushinda.

“Wachezaji wamekubaliana kupata ushindi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza kimataifa hivyo mashabiki wasiwe na presha wawe pamoja nasi kila hatua kwenye mechi zetu.

“Ushindani ni mkubwa na tunajua kwamba hakuna ambaye anapenda kuona  tunakwama hivyo kila mmoja azidi kuwa pamoja nasi,” amesema Kamwe.

Miongoni mwa mastaa wa Yanga ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye safu ya ushambuliaji ni pamoja na Fiston Mayele mwenye mabao matatu ndani ya ligi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here