Home KIMATAIFA YANGA YATINGA MAKUNDI KIMATAIFA UGENINI

YANGA YATINGA MAKUNDI KIMATAIFA UGENINI

0

YANGA wameandika historia kwa kupata ushindi ugenini na kutinga hatua ya makundi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Ushindi pekee umepatikana kipindi cha pili kupitia kwa kiungo wa Yanga Aziz KI ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa leo.

Dakika 45 za awali ni beki Kibwana Shomar alikuwa ni mwiba kwa wapinzani wao Club Africain ambapo alipiga mashuti mawili ambayo yalilenga lango.

Kiungo Bernard Morrison na Sure Boy walikuwa na kazi kubwa uchezesha timu ya Yanga iliyocheza soka la pasi nyingi kipindi cha kwanza na cha pili.

Bao la ushindi limepachikwa dakika ya 79 kwa nyota huyo kuwatungua Waarabu wa Tunisia kwa shuti lilimshinda mlinda mlango.

Pongezi kwa kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui ambaye alifanya kazi kubwa kuweka lango salama dakika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here