Home KITAIFA AZAM FC HESABU ZAO KWA NAMUNGO, NGOMA YAPELEKWA MBELE

AZAM FC HESABU ZAO KWA NAMUNGO, NGOMA YAPELEKWA MBELE

0

MABOSI wa Azam FC wameanza hesabu kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC.

Huo ni mchezo wa mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Awali mchezo huo dhidi ya Namungo ulitarajiwa kuchezwa Jumamosi ya Mei 13 lakini umepelekwa mbele kwa muda wa siku moja ngoma itapigwa Mei 14 palepale Chamazi.

Katika mzunguko wa kwanza mchezo uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, ubao ulisoma Namungo 0-1 Azam FC mtupiaji akiwa ni Edward Manyama.

Ongala ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanatambua utakuwa mgumu.

“Tunatambua aina ya wapinzani wetu ambao tutakutana nao kikubwa ni kufanya maandalizi mazuri na kutumia nafasi ambazo tutazipata,”.

Mchezo uliopita Azam FC ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ukisoma Ruvu Shooting 1-3 Azam FC watupiaji wakiwa ni Ayoub Lyanga aliyetupia mabao mawili na Sopu bao moja wakitumia pasi za Prince Dube na Idris Mbombo ambao ni washambuliaji.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here