Home KITAIFA AZAM FC WANA TAJI MOJA MKONONI LIKIYEYUKA NDO BASI TENA

AZAM FC WANA TAJI MOJA MKONONI LIKIYEYUKA NDO BASI TENA

0

HAKUNA Prince Dube, hakuna Ayoub Lyanga hata Abdul Suleiman, ‘Sopu’ naye ndani ya kuwania tuzo za Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Wakati mwingine tuzo huwa zinakuwa ni kipimo cha ubora na muda mwingine ni kipimo cha kuongeza hasira za mapambano.

Haina maana kwamba wachezaji wa Azam FC hawana ubora haina maana kwamba waliotajwa kwenye tuzo wote ni bora hapana kuna jambo linapaswa kufanyika na wachezaji pamoja na timu kiujumla.

Kwenye upande wa washambuliaji Azam FC namba moja wao ni Idris Mbombo mwenye mabao 7 kagotea hapo kwa muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Kwa wakali wa kutengeneza pasi ni Ayoub Lyanga naye katengeneza pasi 7 za mwisho hapo bado kuna jambo linapaswa kuongezwa kwa Azam FC pamoja na wachezaji kiujumla.

Labda unaweza ukazungumzia upande wa kipa, bado Azam FC haina uhakika na kipa namba moja ni nani Ahamda, Abdulai wote wanapambana kwenye kuonyesha ubora wao.

Kazi bado haijaisha wakati mzuri unakuja lakini kipi kimewakuta Azam FC msimu huu, timu bora bidhaa bora inapambana nafasi ya tatu.

Moja ya timu zinazocheza kwa nidhamu, benchi bora labda maamuzi yanakuwa hayapo upande wao inawezekana lakini ni muda wa kujipanga upya na kufanya kilicho bora.

Mkononi wana fainali moja ya Shirikisho dhidi ya Yanga, wakikwama hapo msimu unayeyuka na wao kabatini hakutakuwa na taji.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here