Home KITAIFA AZAM FC YAIVUTIA KASI COASTAL UNION

AZAM FC YAIVUTIA KASI COASTAL UNION

0

AZAM FC chini ya Kali Ongala imeanza maandalizi kuelekea mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara.

Timu hiyo itakuwa ugenini dhidi ya Coastal Union, utakaochezwa Uwanja Mkwakwani, Tanga, Mei 24 mwaka huu saa 10.00 jioni.

Azam FC mchezo wake uliopita ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 1-2 Namungo FC.

Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala amesema kuwa kazi kubwa ambayo wanaifanya kwa sasa ni kufanyia kazi makosa ambayo walifanya mchezo uliopita.

“Mchezo uliopita kwenye ligi tulifanya makosa jambo lililofanya tukaadhibiwa hivyo kwa sasa tunafanyia kazi ili kupata matokeo mchezo wetu ujao,”.

Miongoni mwa wachezaji wa Azam FC ambao wameanza mazoezi ni pamoja a James Akamiko,Prince Dube,Idrisu Abdulai.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here