Home KITAIFA AZAM YAKUBALI KUWA WALIFELI NA WALISTAHILI KUADHIBIWA NA NAMUNGO

AZAM YAKUBALI KUWA WALIFELI NA WALISTAHILI KUADHIBIWA NA NAMUNGO

0

KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Kali Ongala amesema kuwa Namungo walistahili kupata ushindi kwenye mchezo wao kutokana na wachezaji wake kucheza chini ya kiwango.

Mei 14 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 1-2 Namungo ambao walitupia kimiani kupitia Hassan Kabunda na Shiza Kichuya huku mchezaji wa Namungo Paterne Counou akijifunga.

Azam FC inabakiwa na pointi 53 nafasi ya tatu huku Namungo FC ikiwa nafasi ya tano na pointi 39 kibindoni huku vinara wakiwa ni Yanga wenye pointi 74.

Tayari Yanga imetangazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2022/23 baada ya kusepa na pointi ambazo hazitafikiwa na timu yoyote.

Ongala amesema:” Wachezaji wangu walicheza chini ya viwango na hicho ndo kilichopelekea sisi kupoteza mchezo huo kwasababu Namungo walikuja wakiwa bora zaidi yetu.

“Tumechukua mchezo huu kama funzo kuelekea mechi yetu ya fainali kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) ambapo tumewekeza nguvu zetu nyingi huko.

“Tutarudi uwanja wa mazoezi kuondoa udhaifu huu mkubwa ambao umekua ukitukumba kwa kipindi kirefu na safari hii lazima tupate ufumbuzi,” amesema Ongala.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here