Home KIMATAIFA BAADA YA KULA SHAVU WYDAD CASABLANCA, SVEN KUKUTANA NA UGUMU HUU KWA...

BAADA YA KULA SHAVU WYDAD CASABLANCA, SVEN KUKUTANA NA UGUMU HUU KWA WAARABU

0

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afika Wydad Casablanca wamemtangaza Sven Vandenbroeck kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo na kuchukua nafasi ya Juan Carlos Garido aliyebwaga manyanga.

Sven aliyekuwa akiifundisha Abha inayoshiriki Ligi Kuu ya Saud Arabia tangu Julai 16 hadi Octoba 8, katika mechi sita alizoiongoza timu hiyo alishinda moja, sare moja na kupoteza nne.

Kocha huyo alishawahi kuifundisha Simba SC mwaka 2019 hadi 2021 kabla ya kutimkia Morocco kuinoa timu ya ya FAR Rabat kabla ya kwenda Saudia.

Pia, kabla ya kutua Wydad kocha Sven hakuwa na timu baada ya kutimuliwa Abha aliyoiongoza mechi sita tu.

Wydad inatarajia kucheza nusu fanali Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuiondosha Simba kwa mikwaju ya penalti dhidi ya wababe wa Afrika Kusini Mamelod Sundowns.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here