Home KITAIFA BABA YAKE MESSI AFUNGUKA JUU YA DILI LA SAUDIA ARABIA

BABA YAKE MESSI AFUNGUKA JUU YA DILI LA SAUDIA ARABIA

0

Baba mzazi wa Lionel Messi, Jorge Messi ameuzima uvumi wa kuwa nyota huyo atasaini dili la Mabilioni ya pesa na Klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia. Kupitia chapisho lake kwenye mitandao ya kijamii, Jorge Messi amekanusha taarifa hizo za Messi kuwa atasaini mkataba wenye thamani ya (£522 million) na mahasimu hao wa Al-Nassr.

“Hakuna chochote ambacho kimefikiwa makubaliano na Klabu yoyote kwa msimu ujao. Tutaamua mwisho wa msimu huu. Hatuja saini chochote, au kukubaliana na yeyote. Ni habari za uzushi kwa kutumia jina la Leo.” ameandika Baba yake Messi ambaye pia ni Wakala wake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here