Uongozi wa timu ya Coastal Union FC ya mkoani Tanga imesema inaandaa utaratibu wa kutafuta vipaji vya wachezaji wa mpira kwaajili ya timu hiyo kwenye msimu ujao 2023/24.
Msemaji wa Coastal Union, Miiraji Al Wandy ametoa ahadi hiyo ya kuchukua wachezaji wachanga wilayani Handeni, walipokuwa wakishuhudia mtanange wa fainali za Moja Kwa Moja Cup ambapo timu ya Vibaoni United iliibuka kidedea.
Katibu wa Coastal Union, Omar Ayoub amesema zoezi hilo litaanza mwezi Julai mwaka huu, ambapo litaanzia wilayani Handeni na baadae wilaya nyingine.
Mfadhili wa mashindano ya Moja kwa Moja Cup, Habib Mbota amewaomba wadau wa soka kujitokeza kusaidia vijana wenye vipaji ili waweze kusonga mbele na kutimiza ndoto zao za kucheza timu kubwa.
Nahodha wa timu ya Vibaoni United, Frank Taimuru amesema vijana wengi vipaji wanavyo changamoto ni kukosa vifaa na wafadhili.
Viongozi mbalimbali wilayani Handeni wameahidi kujitokeza kuhakikisha wanaungana kunyanyua vipaji vya soka kwa vijana hao.