Home KITAIFA FEISAL BADO ANAPOKEA MSHAHARA YANGA, ILAA…

FEISAL BADO ANAPOKEA MSHAHARA YANGA, ILAA…

0

Rais wa Klabu ya Yanga (@yangasc) Eng. Hersi Said leo amefanya mahojiano na Kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM ambapo alipata fursa ya Kuzungumza mengi kuihusu Yanga na mafanikio yake lakini pia sakata la Kiungo Feisal Salum ambalo linaendelea.

Eng. Hersi amesema, bado Yanga inamlipa Feisal Mshahara lakini kuna walakini ulitokea mwezi Januari kwenye akaunti yake ya benki

“Feisal bado anaendelea kupokea Mshaharaa Yanga, amepokea hadi mwezi January, lakini baada ya hapo akaunti yake ilianza kuwa na shida kwa kuwa inarejesha pesa ila kila mwezi tunamuingizia pesa lakini zinarudishwa na ushahidi tunao, tumeomba akaunti mbadala ili tumuwekee pesa zake, atakapo tupa akaunti hiyo sisi tutamuingizia pesa zake zote.” – Rais wa Yanga Eng. Hersi Said.

Aidha (@caamil_88) alianika wazi kwamba, Feisal ni mchezaji mwenye nidhamu kubwa sana tangu anajiunga na Yanga. Na kama Klabu ilianza kuboresha Maslahi yake ambapo mwaka 2020 alikuwa akipokea Mshahara wa TSh 1.5 MILIONI na baadaye ulipanda hadi TSh. MILIONI 4 pia wakaboresha Ada yake ya usajili na kufikia TSh. MILIONI 100.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here