Klabu ya Yanga imeanza mazungumzo ya kuinasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Cape Town city ya South Africa, Khanyisa Mayo mwenye umri wa miaka (24).
Mshambuliaji huyo ni kinara wa mabao wa Ligi Kuu ya South Africa msimu huu akiwa na mabao (12) sawa na Peter Shalulile wa Mamelodi Sundowns.
Khanyisa Mayo ambaye pia anaauwezo wa kucheza winga pia anatajwa kuja kuziba nafasi ya Benard Morrison ambaye anatajwa kuwa hataongezewa mkataba kwa msimu ujao
Taarifa zinadai kuwa, Mayo pia emekuwa kwenye Rada za Mabingwa wa Ligi hiyo Mamelod Sundowns hivyo kufanya dili hilo kuwa gumu kiasi kwa upande wa Yanga.
Rais wa Yanga amesema; “Tutamsajili mshambuliaji mmoja kutoka hapa Nchini Afrika kusini msimu huu, ni mapema kumtaja, lakini niwaahidi tu kuwa ni mshambuliaji hatari anayefanya vizuri kwa sasa,” amesema Eng. Hersi Said ambaye ni Rais wa Yanga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE