Home KITAIFA HUU HAPA UKWELI KUHUSU ISHU YA CHAMA KUONDOKA SIMBA

HUU HAPA UKWELI KUHUSU ISHU YA CHAMA KUONDOKA SIMBA

0

WAKATI taarifa zikizagaa kuwa mwamba wa Lusaka, kiungo wa Simba Clatous Chama ameomba kuondoka hofu imeondolewa na uongozi wa timu hiyo.

Kwenye msimamo Simba ipo nafasi ya pili na pointi zao ni 67 na vinara ni Yanga wenye pointi 71.

Yanga imecheza mechi 27 na Simba imecheza mechi 28 msimu wa 2022/23.

Taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa Clatous Chama aliamua kuwaandikia barua ya kuwaaga viongozi wa timu hiyo ikieleza kuwa hatakuwa sehemu ya wachezaji watakaocheza ndani ya Simba msimu ujao.

Kwa sasa Simba imepanga kufanya maboresho katika kikosi hicho ambapo imepanga kufanya usajili mkubwa na wa kisasa utakaowapa nguvu kutinga hatua ya Nusu Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ikumbukwe kwamba msimu huu imegotea hatua ya robo fainali ilipoondolewa na Mabingwa watetezi wa taji hilo Wydad Casablanca.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hizo ni tetesi pekee ambazo mashabiki wa timu hiyo wanapaswa kuachana nazo.

Ameongeza kuwa mashabiki wanapaswa kuelekeza nguvu katika michezo iliyobaki kwenye ligi.

Kiongozi huyo ameweka wazi kuwa hawajapokea barua yoyote kutoka kwa Chama ya kuomba kuondoka hivi karibuni huku wakiendelea na kambi kwa mechi zao.

“Hizo taarifa za Chama kuandika barua Kwa uongozi kuomba kuondoka mara baada ya ligi kumalizika nazisikia lakini kwa uongozi bado hazijafika.

“Niwaondoe hofu mashabiki wa Simba kuwa Chama ni mchezaji wetu na ataendelea kuwepo hapo kwani ana mkataba bado wa mwaka mmoja ndani ya timu.

Mei 12,2023 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Simba 3-0 Ruvu Shooting, Chama alianza kikosi cha kwanza na kutupia bao moja.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here