Home KITAIFA IHEFU HAWANA JAMBO DOGO, WALIOBAKI WAPOKEA CHA MOTO

IHEFU HAWANA JAMBO DOGO, WALIOBAKI WAPOKEA CHA MOTO

0

UONGOZI wa Ihefu umeweka wazi kuwa mechi tatu zilizobaki watacheza kwa umakini kupata pointi tatu.

Timu hiyo ipo nafasi ya 8 ikiwa imekusanya pointi 33 huku vinara wa ligi wakiwa ni Yanga wenye pointi 71.

Zote zimebakiza mechi tatu mechi ijayo kwa Yanga ni dhidi ya Dodoma Jiji na kwa Ihefu ni dhidi ya Coastal Union pale Tanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Mchezo uliopita Ihefu ilipoteza pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania ubao uliposoma Polisi Tanzania 2-1 Ihefu ambapo bao la Ihefu lilifungwa na Adam Adam.

Peter Andrew Ofisa Habari wa Ihefu amesema maandalizi yapo sawa kuelekea mechi ambazo zimebaki.

“Tuna mechi ngumu mbele yetu na tunazidi kufanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kupata matokeo chanya, wachezaji na benchi la ufundi wapo tayari.

“Kikubwa ni kwa mashabiki kuendelea kuwa pamoja nasi tunawashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi wazidi kuwa nasi bega kwa bega,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here