Home KITAIFA JOB NI MVUJA JASHO KINOMANOMA

JOB NI MVUJA JASHO KINOMANOMA

0

BEKI mzawa Dickson Job ndani ya kikosi cha Yanga ameweka rekodi ya kuwa mvuja jasho namba moja kwa wachezaji katika eneo la ukabaji.

Nyota huyo kacheza mechi 22 akivuja jasho ndani ya dakika 1,890 kwenye kuipambania nembo ya jezi ya Yanga katika mechi za Ligi Kuu Bara.

Job kutoka zilipo safu za milima ya Uluguru pale Morogoro ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia.

Ndani ya dakika hizo alizovuja jasho katupia bao moja ilikuwa dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa kwa pigo la kichwa akitumia pigo la kona ya Djuma Shaban.

Ilikuwa ni Februari 4 dakika ya 43 akiwa ndani ya 18 alitimiza majukumu yake kisha akarejea kwenye eneo lake la ulinzi na baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 2-0 Namungo.

Mshikaji wake wa karibu Kibwana Shomary ni mechi 20 amecheza na kusepa na dakika 1,618 na ametupia bao moja pia.

Katika mabao 56 ambayo yamefungwa na Yanga mabeki hawa wawili wazawa wamehusika kwenye mabao mawili na hakuna ambaye ametoa pasi ya bao msimu huu wakati Yanga ikisepa na ubingwa na pointi zao kibindoni ni 74 na kuna mechi mbili mkononi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here