Home KITAIFA KINAWAKA LEO NUSU FAINALI SINGIDA BIG STARS V YANGA

KINAWAKA LEO NUSU FAINALI SINGIDA BIG STARS V YANGA

0

BENCHI la ufundi la Singida Big Stars limeweka wazi kuwa lipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa nusu fainali Azam Sports Federation dhidi ya Yanga.

Timu hiyo inayonolewana Kocha Mkuu, Hans Pluijm inapambana na mabingwa watetezi wa taji hilo Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Pluijm amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo wa leo na wataingia kwa tahadhari kupata ushindi ili watinge hatua ya fainali.

“Wapinzani wetu tunatambua ni timu bora na kila timu inahitaji ushindi hivyo tutaingia kwa tahadhari kutafuta ushindi na tulipata muda wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu,” .

Cedrick Kaze kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa wanatambua uimara wa wapinzani wao wataingia kwa tahadhari kupata ushindi.

“Kila mchezaji anatambua uimara wa wapinzani wetu licha ya ratiba kuwa ilivyo haiwezi kuwa sababu tutaingia wa hesabu za kusaka ushindi,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here