Home BOXING KISA MATOKEO YA TWAHA KIDUKU, MWAKINYO ASHINDWA KUJIZUIA, ATAJA WANAOMFELISHA

KISA MATOKEO YA TWAHA KIDUKU, MWAKINYO ASHINDWA KUJIZUIA, ATAJA WANAOMFELISHA

0

Bondia mashuhuri nchini, Hassan Mwakinyo ‘Champez’, amelalamikia viongozi wa Kamisheni ya kusimamia ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), kwa kile alichodai kuwa viongozi hao wanafanya kazi kwa ubaguzi, jambo ambalo linalokwamisha maendeleo ya mchezo huo nchini.

Kauli hiyo ya Mwakinyo inakuja kufuatia matokeo ya pambano lake la April 23 uwanja wa Jamhuri Dodoma dhidi ya Kuvesa Katembo kutowekwa kwenye mtandao unaohifadhi rekodi na takwimu za mabondia wote Duniani (Boxrec), huku matokeo ya bondia Twaha Kiduku aliyecheza April 22 yakiwekwa.

“Viongozi wa chama cha ngumi za kulipwa Tanzania wanafanya kazi kwa kubagua sana watu, hili ni tatizo ambalo linaendelea kwa kasi kubwa sana, that’s why wakati mwengine naamua kujitenga sababu ya unafiki uliopo.

“Pambano letu linamaliza week ya 3 sasa matokeo hayaja wekwa boxrec mpaka leo kwa sababu ambazo hazina msingi wala mashiko support ya chochote hamna tunajikwamua wenyewe bado mnatuonyesha jealousy za kutukwamisha kwenye mipango yetu.

“Nakuomba waziri mwenye dhamana ya michezo na Naibu waziri mufanye maamuzi ya haraka kwenye hili haki itendeke huu sio utanga na udar hili ni taifa la tanzania” aliandika Mwakinyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here