Home KITAIFA KOCHA JULIO KAANZA MIKWARA

KOCHA JULIO KAANZA MIKWARA

0

KOCHA Mkuu wa KMC, Jamhuri Kihwelo, ‘Julio’ ameanza mikwara kwa kubainisha kuwa kinachotazamwa kwenye ligi ni namna ya kumaliza.

Mbele ya Singida Big Stars inayonolewa na Hans Pluijm ilisepa na pointi tatu mazima.

Ikumbukwe kwamba mchezo wake wa pili kukaa benchi akiwa na KMC baada ya kubeba mikoba ya Thiery Hitimana  amesepa na pointi tatu.

Ubao wa Uwanja wa Uhuru baada ya dakika 90 Mei 12 ulisoma KMC 2-0 Singida Big Stars.

Mchezo wa kwanza ilikuwa ugenini alishuhudia ubao wa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma ukisoma Dodoma Jiji 1-0 KMC.

Kwa ushindi aliopata KMC inafikisha pointi 29 nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 28.

“Bado ambacho kinatazamwa kwenye ligi ni namna ambavyo utamaliza kwa kuwa kikubwa ni kupata ushindi na kila mmoja anapambana kupata ushindi.

“Pongezi kwa wachezaji kwa namna ambavyo wanapambana na kwa mechi ambazo zimebaki tuna amini kwamba tutapata matokeo chanya na kubaki ndani ya ligi,”.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here