Home KITAIFA KOCHA ONGALA KAWAZIDI SIMBA NJE NDANI

KOCHA ONGALA KAWAZIDI SIMBA NJE NDANI

0

MBINU za Kali Ongala muda wote zimekuwa ngumu dhidi ya Simba wanapokutana ndani ya dakika 90.

Ongala dhidi ya Yanga alikwama kusepa na pointi mzunguko wa pili ila ule mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Mbele ya Singida Big Stars ugenini walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Ni bao moja Simba wamefanikiwa kuifunga Azam FC chini ya Ongala ilikuwa mchezo wa hatua ya nusu fainali Azam Sports Federation na mtupiaji akiwa ni Sadio Kanoute.

Kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara hakuna staa wa Simba aliyefanikiwa kuifunga Azam FC.

Kwenye sare ya kufungana bao 1-1 ni Abdala Kheri beki wa Azam FC kwenye harakati za kuokoa alijifunga na kufanya wagawane pointi mojamoja.

Simba mchezo wake wa kwanza kupoteza ndani ya ligi msimu wa 2022/23 ni dhidi ya Azam FC na mchezo wake wa kwanza kupoteza kwenye Azam Sports Federation ni dhidi ya Azam FC Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here