Home KITAIFA KUHUSU SAKATA LAO NA FEI TOTO, YANGA WAPEWA NJIA HII NYEPESI YA...

KUHUSU SAKATA LAO NA FEI TOTO, YANGA WAPEWA NJIA HII NYEPESI YA KUMALIZA KESI KWA USHINDI

0

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Ibra kasuga amesema kuwa Klabu ya yanga wanapaswa kumshitaki mchezaji wao Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ kwa kukiuka matakwa ya mkataba wake na kutoroka kambini.

Kasuga amesema hayo kufuatia kesi ya Fei Toto na Yanga SC kushindwa kutolewa maamuzi jana na badala yake itatajwa baadaye na TFF.

Fei Toto ambaye aliandika barua Desemba 2022, akidai kuwa amevunja mkataba na klabu yake hiyo licha ya klabu kukataa na fukuto linaendelea TFF mpaka sasa.

“Kwa sasa naweza kusema Yanga ni wazembe kwenye kesi yao hii na mchezaji Feisal, kwa sababu maamuzi yalishatolewa mara mbili na TFF na wao wameshinda lakini bado wanashindwa kufungua kesi mpya ya mchezaji kutokuonekana kazini.

“Wakiitwa na kwenye kesi wanakubali kwenda wakati Feisal Salum ni mali yao halali na anatakiwa kuwepo kambini ili kukubaliana aidha kuvunja mkataba au kumuongezea mkataba,” Ibra Kasuga.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here