Makamu wa Rais wa klabu ya wananchi Young Africans, Arafat Haji amehamasisha watanzania, taasisi na sekta mbali mbali katika nchi yetu kuamini katika kuwapa nafasi vijana katika nyanja tofauti tofauti.
Akiwa katika mahojiano amesema “Kuna dhana bado Tanzania ipo ya kutoamini katika vijana, lakini kwa sasa kupitia Yanga wameanza kuona na kuamini kuwa vijana wakiaminiwa wanaweza.
Ukiingalia Yanga kuanzia uwanjani hadi kwenye uongozi utaona vijana wengi, tuna lengo moja bila kujali umri na tunahakikisha linatimia kwa nguvu zote.
Mpira kwa sasa ni sayansi na sio maneno tu na mambo mengine hivyo unahitaji wataalamu na watu wenye taaaluma katika uongozi na masuala mengine ya kitimu.” Arafat Haji, Makamu wa Rais Yanga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE