Home KITAIFA MAKIPA BONGO MAKOSA MUHIMU KUFANYIA KAZI

MAKIPA BONGO MAKOSA MUHIMU KUFANYIA KAZI

0

MAKIPA wengi wamekuwa wakiingia kwenye lawama kutokana na kufungwa mabao ambayo yanaleta maswali baada ya mchezo husika.

Hii imekuwa ikiwakumba makipa wote wale wageni na hawa makipa wazawa nao wamekuwa kwenye kasumba hii jambo ambalo halipendezi.

Ukweli upo wazi kwamba mpira ni mchezo wa makosa lakini yanapozidi ni muhimu kufanyia kazi na kila mmoja kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Makipa ni muda wao kuendelea kuongeza umakini na kufanyia kazi makosa ambayo wamefanya kwenye mechi ambazo zimepita hii itawafanya wawe bora zaidi.

Katika mzunguko wa kwanza tuliona namna makipa ambavyo walikuwa wakiingia kwenye migogoro na viongozi wao na wapo ambao waliomba kuondoka kwenye timu zao.

Haina maana kwamba uwezo hawana wanao ila makosa yalikuwa yamezidi na mwisho viongozi wakahitaji kuona mabadiliko hasa kutokana na matokeo kuwa mabovu.

Mzunguko wa lala salama upo kwa sasa na kila timu inapambana kusaka pointi tatu hivyo ni muhimu kila mmoja kufanya kazi yake kwenye nafasi yake.

Makipa ni sehemu muhimu kutimiza majukumu katika kuzuia mpira usizame kwenye nyavu na hii itawafanya watimize majukumu kwa umakini.

Safu ya ulinzi ni muda wa kuongeza umakini katika kulinda ngome isifungwe kwani mashabiki wanaojitokeza wanahitaji kuona ushindi.

Yote kwa yote kila mmoja ni wakati wake kutimiza majukumu yake hapana muda wa kupoteza bali umakini uzingatiwe.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here