Home KIMATAIFA MAMELODI MWENDO UMEGOTA, WAARABU HAO FAINALI

MAMELODI MWENDO UMEGOTA, WAARABU HAO FAINALI

0

MAMELODI Sundowns ya Afrika Kusini imegotea katika hatua ya nusu fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Sare ya kufungana mabao 2-2 Wydad Casablanca Waarabu kutoka Morocco imewaondoa kwenye reli wababe kutoka Afrika Kusini.

Ni mabao ya Themba Zwane dakika ya 50 na Peter Shalulile dakika ya 79 kwa upande wa Mamelodi Sundowns ilikuwa hivyo.

Wydad Casablanca ni Ayoub El Amloud dakika ya 72 alianza kuweka usawa na Mathobi Mvala hakuwa na bahati katika harakati za kuokoa alijifunga dakika ya 83.

Wydad Casablanca wanasonga mbele mpaka hatua ya fainali Kwa faida ya mabao ya ugenini waliyopata Uwanja wa Loftus Versfeld.

Ni Sven Vandebroeck alikuwa benchi la Wydad Casablanca na kubainisha kuwa uzoefu umewabeba na wanakwenda kucheza na Al Ahly katika fainali.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here