Home KITAIFA MASHABIKI NA WANACHAMA WA SIMBA SC, WAOMBWA RADHI

MASHABIKI NA WANACHAMA WA SIMBA SC, WAOMBWA RADHI

0

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salim Abdallah ‘Try Again’ amewaomba radhi Wanachama na Mashabiki wa klabu hiyo kwa kushindwa kutwaa taji lolote ikiwa ni msimu wa pili mfululizo.

Try Again aliyasema hayo jana Ijumaa (Mei 12) akieleza kuwa kwenye mpira hali hiyo ni ya kawaida na haipaswi kunyoosheana vidole katika kipindi hiki na badala yake wanapaswa kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Klabu Simba SC ambayo jana iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inakaribia kuupoteza ubingwa wa Ligi hiyo endapo Young Africans itashinda mechi yake dhidi ya Dodoma Jiji itakayopigwa leo Jumamosi (Mei 13).

Akifafanua kilichowaangusha kukosa makombe hayo, Try Again alisema ni majeraha yaliyokuwa yakiwaandama wachezaji wao, wachezaji wapya waliowasajili walioshindwa kuonesha ubora na ugumu wa mechi za Ligi Kuu.

“Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, nachukua nafasi hii kuwaomba radhi Wanasimba wote, hatukuwa na msimu mzuri sababu tumekosa mataji yote.

Tumekuwa na changamoto ya majeruhi kikosini, wale tuliowaongeza pia wameshindwa kuonesha ubora lakini ndio mpira tunajipanga kwa msimu mpya,” amesema Try Again

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here