Home KITAIFA MDAKA MISHALE KAWAKIMBIZA KINOMANOMA

MDAKA MISHALE KAWAKIMBIZA KINOMANOMA

0

DJIGUI Diarra, kipa namba moja wa Yanga amewakimbiza wapinzani wake wote kwenye kucheza mechi nyingi bila kufungwa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Anapambania tuzo yake ya kuwa kipa bora msimu uliopita aliyosepa nayo alipokuwa akishindana na kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.

Msimu huu wa 2022/23 Djigui ni mechi 24 kacheza kwenye ligi akisepa na dakika 2,127 akiwa hajafungwa kwenye jumla ya mechi 16.

Ni mabao 12 Djigui katunguliwa katika hayo ni Abdul Suleiman, ‘Sopu’ anashikilia rekodi ya kumtungua mabao mengi kwenye mchezo mmoja ambayo ni mawili.

Anayemfuatia kwa kutofungwa mechi nyingi ni mshikaji wake Aishi Manula wa Simba ambaye hajafungwa kwenye jumla ya mechi 12 za ligi.

Kwa sasa Manula anapambania afya yake baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhihi ya Ihefu, uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Kuna uwezekano mkubwa wa nyota Djigui kusepa na tuzo hiyo kwa mara nyingine kutokana na kasi aliyonayo na mechi tatu mkononi zinawafuata Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 71 kibindoni.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here