Home KITAIFA MIPANGO YA IHEFU NI KUFANYA “UMAFIA” KAMA WALIO WAFANYIA YANGA

MIPANGO YA IHEFU NI KUFANYA “UMAFIA” KAMA WALIO WAFANYIA YANGA

0

UONGOZI wa Ihefu umebainisha kuwa umeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Coastal Union.

Ihefu inashikilia rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga Yanga msimu wa 2022/23 walipokutana Uwanja wa Highland Estate mzunguko wa kwanza.

Mzunguko wa pili Yanga walilipa kisasi kwa kuitungia Ihefu bao 1-0 Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Mei, 13 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ikiwa ni mzunguko wa pili.

Ofisa Habari wa Ihefu, Peter Andrew amesema kuwa tayari kikosi kipo kambini kwa ajili ya maandalizi kwa mechi ijayo dhidi ya Coastal Union,

“Tupo kwenye mchakato wa kutafuta  mechi mbili za kirafiki ambazo hizo zitawafanya wachezaji wawe fiti na imara kwa ajili ya mechi zijazo kwa kuwa wachezaji tayari wapo kambini kwa program maalumu.

“Mechi za kirafiki zitaongeza nguvu na utimamu wa mwili kwa wachezaji na hali ya wachezaji inazidi kuimarika kwa kuwa ari ni kubwa wale ambao walikuwa ni majeruhi wamepona na wamerejea kikosini,” amesema Andrew.

Kwenye msimamoa Ihefu ipo nafasi ya 8 ina pointi 33 baada ya kucheza mechi 27.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here