Home KITAIFA MTIBWA SUGAR MKIA WAKE MGUMU

MTIBWA SUGAR MKIA WAKE MGUMU

0

MTIBWA Sugar mkia wao wanaokula ni mgumu kutokana na kuwa ni namba moja kwa timu iliyotunguliwa mabao mengi zaidi ndani ya ligi.

Yanga na Simba zinaogoza kwa timu ambazo zimefungwa mabao machache msimu huu wa 2022/23 baada ya mechi 28.

Yanga imefungwa mabao 15 sawa na yale ambayo imefungwa Simba.

Timu zote zikiwa zimecheza jumla ya mechi 28 ni mabao 44 wameokota kwenye nyavu zao huku safu ya ushambuliaji ikifunga mabao 28.

Ndani ya dakika  2,520  wana wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 57 ndani ya ligi huku ile ya ushambuliaji ikiwa ina wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 90.

Kwenye msimamo Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ina pointi 29 na mechi mbili imebakiwa nazo.

Ni Simba inaongoza kwa timu yenye mabao mengi ya kufunga ndani ya ligi ambayo ni 66 ndani ya dakika 2,520 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 38.

Yanga na Simba ni timu pekee ambazo zimefungwa mabao machache ambayo ni 15 wakiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika ya 168.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here