Home KITAIFA POLISI TANZANIA YAGOMEA KUSHUKA DARAJA

POLISI TANZANIA YAGOMEA KUSHUKA DARAJA

0

KOCHA msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema kuwa wanatambua ushindani uliopo kwenye ligi ni mkubwa watapambana kushinda mechi zilizobaki ili kufufua matumaini ya kubaki ndani ya ligi.

Vinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga ambao wametwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo wakiwa na pointi 74 na wana mechi mbili mkononi.

Polisi Tanzania ikiwa imecheza mechi 28 imekusanya pointi 25 ikiwa nafasi ya 15, Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 16 tayari imeshashuka rasmi daraja.

Tamba aliweka wazi kuwa mechi zilizobaki ni za maamuzi kwao jambo watakalochukulia umakini kupata ushindi.

“Tuna mechi mbili ambazo zimebaki mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao tumepata pointi tatu huo umeisha hivyo kwa sasa tunaanza maandalizi ya mechi zetu zijazo.

“Kikubwa ni kupata ushindi kwanza hapo tutakuwa na nafasi ya kuendelea kubaki kwenye ligi na tunajua ushindani ulivyo nasi tutaingia kwenye mechi hizo kwa ushindani mkubwa.

“Tunatambua ushindani ambao upo kwenye ligi nasi tutafanya maandalizi mazuri ili kupata matokeo mazuri ndani ya dakika 90,”.

Ni Ruvu Shooting tayari imeshuka daraja jumlajumla msimu wa 2022/23 ikiwa imebakiwa na mechi mbili za kucheza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here