Home KITAIFA SIMBA KUJA KIVIGINE TENA MASHINDANO YAJAYO

SIMBA KUJA KIVIGINE TENA MASHINDANO YAJAYO

0

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa utakuja kivingine ndani ya msimu mpya wa 2023/24 kwa kuleta wachezaji wenye sifa ya ushindani na kutafuta matokeo bila kukata tamaa.

Katika anga la kimataifa wamegotea hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika na watani zao wa jadi Yanga wapo hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwenye ligi Simba imegotea nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 28 ina pointi 67 mabingwa ni Yanga wenye pointi 74 kibindoni.

Salim Abdallah, ‘Try Again’ Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba amesema kuwa watafanya kazi kubwa kwenye maboresho ya kikosi kwa kuwaongeza wachezaji wazuri watakaoleta ushindani.

“Haikuwa msimu mzuri kwetu 2022/23 ambacho tunakifanya kwa sasa ni kuangalia pale ambapo tulikwama na kuboresha kikosi kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zetu msimu ujao.

“Yaliyotokea tumeona na kwa sasa tunafanyia kazi kwani mpira una mambo mengi yanatokea nasi tunazidi kujiimarisha kuwa kwenye mwendo mzuri utakaotufanya tuje kivingine,”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here