Home KITAIFA SIMBA KUWAPA FURAHA MASHABIKI

SIMBA KUWAPA FURAHA MASHABIKI

0

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema kuwa watautumia mchezo wao wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting kuwapa furaha mashabaki.

Timu hiyo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya pointi 64 vinara ni Yanga wenye pointi 71.

Yanga na Simba zote zimecheza mechi 27 na ni mechi tatu zipo kwenye mikono yao kukamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2022/23.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.

Bocco amesema:”Tunafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Ruvu Shooting tunatambua kwamba utakuwa ni mgumu lakini tupo tayari kuwapa furaha mashabiki.

“Tunawashukuru kwa namna ambavyo wamekuwa pamoja nasi kwenye mechi ambazo tunacheza na tunatambua umuhimu wa mashabiki tutapambana kuwapa furaha,”.

Ndani ya ligi John Bocco amefunga mabao 9 akiwa na pasi moja ya bao mshikaji wake Mohamed Hussein ambaye ni nahodha msaidizi katoa pasi tano za mabao.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here