Mels Daalder Skauti Mkuu Simba SC, UONGOZI wa Klabu ya Simba SC, umemteua Mels Daalder Raia wa Uholanzi kuwa msaka vipaji (Skauti Mkuu) ambaye ana uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali.
Mels ameshiriki kozi mbalimbali za Duniani ikiwa ni pamoja na zilizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.
Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na anaijua vizuri Ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula amesema kuwa eneo la skauti ni muhimu ingawa lilikuwa haipewi nafasi kubwa na kwa kuliona hilo tumeamua kumleta Mels.
” Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye skauti kwakuwa ni eneo muhimu katika mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa,” amesema Kajula.
Mels Daalder Skauti Mkuu Simba SC, Simba yasajili mtaalamu wa kusaka vipaji.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE