Home KITAIFA SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTIMG, YASHUKA DARAJA

SIMBA YAICHAPA RUVU SHOOTIMG, YASHUKA DARAJA

0

KLABU ya Ruvu Shooting imeshuka daraja rasmi kutoka Ligi Kuu Bara hadi Championship (Ligi Daraja la Kwanza) msimu ujao baada ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Simba katika mchezo wa 28 msimu huu uliochezwa Azam Complex, Chamazi.

Mabao ya Simba yamefungwa na Clatous Chama dakika ya 30, Pape Sakho dakika ya 72 na 90 akitumia pasi za Saido Ntibanzokiza.

Matokeo hayo yanaifanya Ruvu ibaki na alama zake 20 mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na mechi mbili mkononi ambazo hata kama itashinda zote, haitaweza kutoka kwenye nafasi mbili za mwisho.

Katika msimamo wa ligi, Ruvu Shooting iko nyuma ya Polisi Tanzania wenye alama 22 na mechi tatu mkononi, ikifuatiwa na Mbeya City wenye alama 27 na mechi tatu mkononi, huku nafasi ya 13 akiwemo Mtibwa Sugar mwenye alama 29 na mechi tatu mkononi.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here