Home KITAIFA TANZANIA PRISONS KUBORESHA NGUVU USHAMBULIAJI

TANZANIA PRISONS KUBORESHA NGUVU USHAMBULIAJI

0

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Abdalah Mohamed,’Bares’ amesema kuwa watafanya kazi kubwa kuiboresha safu ya ushambuliaji ili kufunga mabao mengi zaidi.

Prisons ipo nafasi ya 9 ina pointi 31 baada ya kucheza mechi 27 katika ligi msimu wa 2022/23.

Ikumbukwe kwamba vinara wa ligi ni Yanga wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 26 za ligi.

Yanga waliwafungashia virago Prisons kwenye mashindano ya Kombe la Azam Sports Federation mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Bares amesema kuwa katika kutafuta ushindi kwenye mechi zilizobaki ni muhimu kufunga mabao mengi kuongeza nguvu ya kujiamini katika mchezo husika.

“Ushindi unahitaji mabao mengi na ukipata kufunga mapema unaongeza hali ya kujiamini hili ni muhimu kwetu na tunalifanyia kazi eneo la mazoezi.

“Katika mechi zilizopita tulikuwa tunapata nafasi lakini tukashindwa kuzitumia ila muda uliobaki tunafanya kazi kwenye makosa ambayo tulifanya kwenye mechi ambazo tumepitia,” amesema Bares.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here