Home KITAIFA USM ALGER: HATUCHEZI NA MAYELE SISI

USM ALGER: HATUCHEZI NA MAYELE SISI

0

ABULEKH Banchikha, Kocha Mkuu wa USM Alger ameweka wazi kuwa mchezo wao wa leo hawatacheza na mshambuliaji Fiston Mayele wa Yanga.

Mayele ni kinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga kwenye anga la kimataifa akiwa ametupia mabao sita.

Yupo sawa na yule wa Marumo Gallants anayeitwa Ranga Chivaviro lakini timu hiyo imegotea hatua ya nusu fainali ilipoondolewa na Yanga.

Kocha huyo amesema:”Sisi hatuendi kucheza na Mayele, tunakwenda kucheza na Yanga.

“Hivyo mfumo wetu ndio tunaokwenda kuutumia kwenye mchezo wetu huo ndio utakaokwenda kumzuia Mayele,”.

Leo Mei 28 mchezo huo wa hatua ya fainali unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here