Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amefunguka kuhusu sakata la ubaguzi ambalo mchezaji wake Vinicius Jr alikumbana kwa mara nyingine tena jana kwenye mchezo dhidi ya Valencia.
Carlo amesema “Vini hakutaka tena kucheza baada ya kitendo kile, nilimwambia yupo sawa kabisa. Nilimwambia mwamuzi asimamishe mchezo, LaLiga kuna tatizo kubwa, ilikuwa ni uwanja mzima unamuita “nyani” na sio mtu mmoja. Mchezo ulipaswa kusimama mara moja.” amekaririwa Kocha Ancelotti.
Aidha baada ya mchezo huo ambao ulishuhudia Vini akioneshwa Kadi nyekundu Dakika ya 90+5, alienda kwenye mtandao wake wa Instagram na kuandika machungu yake akisema, Ligi ambayo wamepita watu kama Ronaldinho, Ronaldo, Messi imegeuka kuwa ya Kibaguzi. Vini ni muhanga wa matukio haya ambapo amekuwa akibaguliwa mara kwa mara kwenye LaLiga.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE