Home HABARI WASIWASI DAWA, WAARABU SIO WA KUWABEZA

WASIWASI DAWA, WAARABU SIO WA KUWABEZA

0

WASIWASI ni dawa wanasema hivyo hivyo kwa wawakilishi kwenye anga la kimataifa Yanga hampaswi kujiamini kupita kiasi.

Mwendo ambao mlianza nao kwenye kila hatua hakika unapaswa kupongezwa na ili uwe na mwendelezo mzuri ni muhimu kupata ushindi leo kwenu Yanga.

Moja ya fainali kubwa na ngumu kupata kutokea ni hii hapa kwa kuwa kosa moja ni mwendo wa kupata maumivu makubwa ambayo yatadumu kwa muda mrefu.

Mchezo wa kwanza unatoa picha nzuri kwa ajili ya mechi zijazo na inawezekana kuwa kwenye mwendo mzuri hata ugenini kwa kuwa picha inaanza kupigwa hapa Uwanja wa Mkapa.

Imani kwa wachezaji ni kubwa kwenye kupambania kombe hasa kwa kupata matokeo mazuri ndani ya dakika 90.

Zile porojo ambazo zilikuwa zinazungumzwa na kila mmoja kwa sasa ni muda wa kuzionyesha kwenye vitendo.

Mashabiki ni muda wa kujitokeza uwanjani kuishangilia timu bila kuchoka kwani uwepo wa mashabiki kunaongeza ngvu kwenye kupambania ushindi.

Kila mchezaji ni muda wake kupambana na kuleta ushindani ndani ya uwanja ili kuwapa furaha mashabiki na furaha kwa Watanzania.

Huu ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili ambazo zinasaka ushindi ndani ya dakika 90 ikawe ni busara kutumia makosa ya wapinzani huku wachezaji wakipunguza makosa ambayo yanaweza kupunguzwa.

Familia ya michezo furaha yao ipo kwenye ushindi hivyo ni kazi kwa wachezaji kuwapa zawadi ya ushindi ikumbukwe kwamba wapinzani wenu USM Alger sio wakuwabeza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here