Home KITAIFA YANGA BINGWA LIGI KUU YA NBC, YAICHAPA 4-2 DODOMA JIJI

YANGA BINGWA LIGI KUU YA NBC, YAICHAPA 4-2 DODOMA JIJI

0

Klabu ya Young Africans SC yatangaza ubingwa wa ligi kuu bara NBC msimu wa 2022/23.

Ni baada ya kuitandika timu ya Dodoma Jiji mabao 4-2 katika uwanja wa Azam Complex, ambapo yanga imefikisha point 74 katika msimamo wa ligi ambapo hakuna tumu yoyote inayoweza kufikia point zake kwa sasa.

Huu ni ubingwa wake wa 29 tangu kuanzishwa kwake katika historia na huku ikiwa ni timu pekee kutoka Tanzania yenye mataji mengi ya ubingwa nchini.

Magoli ya Yanga katika mchezo wa leo yamewekwa kambani na Kennedy Musonda katika dakika ya 39, Mudathir Yahya dakika ya 71′ na 90’+4 pamoja na Farid Mussa katika dakika ya 88′.

Huku mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na Collins Opare katika dakika ya 59′ pamoja na Seif Karihe kwenye dakika ya 67′.

Yanga bingwa

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here