Home KIMATAIFA YANGA KAMILI KUIVAA MARUMO KIMATAIFA

YANGA KAMILI KUIVAA MARUMO KIMATAIFA

0

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa maandalizi ya kuwakabili wapinzani wao Marumo Gallants yanakwenda sawa.

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi tayari kimetia timu Afrika Kusini kwa mpango kazi wa kusaka ushindi Mei 17.

Mchezo huo ni hatua ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mshindi wa jumla atatinga hatua ya fainali.

Yanga imetanguliza mguu mmoja kuelekea fainali kwa kuwa na faida ya mabao 2-0 iliyopata kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Mkapa.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wapo tayari.

“Baada ya kuwasili Afrika Kusini benchi la ufundi lilianza mipango yake kwa ajili ya mchezo wetu wa pili na tunatambua utakuwa mchezo mgumu kutokana na ushindani ambao upo.

Dua kwa mashabiki waliopo Tanzania na Afrika kiujumla na wale watakaoungana nasi kwenye mchezo tunasema ni muda wetu wa kuishangilia timu yetu,”.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini ni Djigui Diarra, Dickson Job, Bacca, Mudhathir Yahya na Fiston Mayele.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here