Home Uncategorized BRUNO BADO YUPO SANA, MIGUEL NDO BASI TENA

BRUNO BADO YUPO SANA, MIGUEL NDO BASI TENA

0

KAZI imeanza ndani ya Singida Fountain Gate ambayo zamani ilikuwa inaitwa Singida Big Stars kwa kutambulisha nyota walioongeza mkataba pamoja na wale watakaosepa ndani ya timu hiyo.

Timu hiyo ni mashuhuda Yanga wakisepa na ubingwa wa ligi huku wao wakigotea nafasi ya nne.

Rasmi Juni 24 walifungua ukurasa wao mpya kwa kuanza kuwataarifu mashabiki kuhu wale watakaokuwa nao na wale ambao hawatakuwa ndani ya kikosi hicho.

Ni Bruno Gomes mtaalamu wa mapigo huru akiwa ametupia jumla ya mabao 10 kibindoni ndani ya Singida Big Stars.

Katka maao hayo 10 kuna mabao mawili alizitungua timu zilizopo tatu bora kwa mapigo huru ikiwa ni Azam FC pamoja na Simba.

Alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za timu za Kariakoo ila mabosi wa Singida Fountain Gate wakaongeza nguvu na kumpa dili la miaka miwili.

Hivyo hatakuwa Yanga wala Simba bado yupo Singida mpaka 2025.

Wakati Bruno akiendelea kuwa ndani ya Singida raia wa Argentina Miguel Escodar kapewa mkono wa asante.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here