Al Ahly imetwaa ubingwa wa 11 Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kupigania dakika 180 za mechi ya fainali nyumbani na ugenini.
Al Ahly ilianza uwanja wa nyumbani nchini Misri kwa ushindi wa 2-1 ambapo walitengeneza mlima mdogo kwao kuupanda kwenye mechi ya ugenini Morocco.
Ikiwa Morocco Al Ahly ilichanga karata zake kwa kutoka sare ya bao 1-1 ikisawazisha baada ya kutanguliwa na wenyeji wao Wydad.
🧏🏾♂️ Al Ahly imekuwa timu ya pili ambayo msimu huu ilimaliza nafasi ya pili kwenye hatua ya makundi michuano ya CAF ikianza USM Alger kwenye Shirikisho ikiwa kundi A ilimaliza nafasi ya pili nyuma ya Marumo Gallants na Al Ahly ilimaliza kundi B nyuma ya Mamelodi Sundowns.