Home KITAIFA DUBE KAFUNGA KIBABE BONGO

DUBE KAFUNGA KIBABE BONGO

0

WAKATI msimu wa 2022/23 ukifungwa mwamba Prince Dube kafunga kwa rekodi ya kusepa na mpira wake wa kwanza msimu huu kwenye ligi.

Dube ambaye anatarajiwa kuwa miongoni mwa nyota watakaocheza fainali ya Azam Sports Federation dhidi ya Yanga alifunga mabao manne peke yake.

Juni 12 Azam FC inatarajiwa kumenyana na Yanga kwenye fainali Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ni dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 8-0 Polisi Tanzania.

Ushindi mkubwa kwa Azam na wa wa kwanza kwenye ligi msimu huu kupita timu zote uwanjani.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KATIKA APP YETU YA SOKALEO >>BONYEZA HAPA<<< KUIDOWNLOAD PLAYSTORE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here